Summary
Read the full fact sheet- Unaweza kumsaidia mtoto wako kupona kutokana na hali ya uzoefu aliyopitia yenye kuhuzunisha au ya kutisha. Uzoefu huu unaweza kujumuisha: ajali za gari, moto wa misitu na mafuriko, ugonjwa wa ghafla au kifo katika familia, uhalifu, unyanyasaji au vurugu.
- Watoto wataangalia: jinsi ya unakabiliana na mgogoro wewe mwenyewe, jinsi unavyoitikia hisia na tabia zao.
- Vidokezo hivi vinaweza kukusaidia kuwa na mazungumzo na mtoto wako kuhusu uzoefu wake. Ni muhimu kumwambia mtoto wako ukweli, kwa njia ambayo anaweza kuelewa kulingana na umri wake.
- Unaweza muda wote kutafuta msaada wa kitaalamu. Mahali pazuri pa kuanzia ni daktari wako wa familia.
On this page
Jinsi watoto wanavyoitikia tatizo la kiwewe
Mwitikio wa mtoto kutokana na uzoefu wa kufadhaisha au wa kutisha unaweza kutegemea:
- miaka yake
- utu wake
- jinsi wewe au familia yako mnavyoitikia
Mtoto wako anaweza asiitikie kwa njia unazotarajia. Wanaweza kuwa:
- kujitenga - wanaweza kupoteza hamu katika shughuli. Wanaweza pia kuwa na ujasiri mdogo, kuwa kimya, au kurudi kwenye njia za tabia wakati alipokuwa mtoto.
- kujishughulisha – wanaweza kuhitaji kuhuisha uzoefu aliopitia. Kwa mfano, kupitia mchezo wa kurudia au michoro. Mtoto wako anaweza kuwa na hofu kuhusu matukio yajayo au anaweza kuwa na ndoto mbaya.
- wasiwasi – wanaweza kuwa na matatizo ya kuzingatia au makini. Wanaweza kutaka kuwa karibu nawe kila wakati, kuwa na matatizo ya usingizi au kufadhaika kwa urahisi.
- kutojisikia vizuri – wanaweza kuwa na maumivu ya kichwa na tumbo.
Mtoto wako anaweza kuwa na mwitikio wa kuchelewa. Watoto wengine wanaweza kuonekana kuwa sawa, lakini wanaweza kuitikia kwa siku, wiki au hata miezi baadaye.
Jinsi ya kuzungumza juu ya tukio linalosababisha kiwewe
Itasaidia mtoto wako ikiwa wewe ni mwaminifu kwake. Unaweza:
- mhakikishie mtoto wako kwamba yuko salama na kwamba tukio limekwisha. Huenda ukalazimika kumhakikishia mara nyingi.
- msikilize mtoto wako. Chukua wasiwasi na hisia zake kwa uzito.
- mjulishe mtoto wako kwamba ungependa kusikia kuhusu jinsi anavyohisi.
- mwambie mtoto wako kuhusu kile kilichotokea kwa njia inayolingana na umri wake. Tumia lugha anayoelewa. Ikiwa mtoto wako hajui mambo ya msingi, anaweza kujaribu kusuluhisha kilichotokea peke yake mwenyewe. Anaweza kutumia mawazo yake au maelezo machache kukamilisha historia. Hii inaweza kusababisha wasiwasi na kuchanganyikiwa zaidi kwa mtoto wako.
- hakikisha mtoto wako anajua siyo kosa lake. Wanaweza kufikiria hivi ikiwa alikuwa mtukutu au alifikiria mambo mabaya juu ya mtu fulani.
- zungumza kuhusu tukio hilo kama familia. Ruhusu kila mtu atoe maoni yake, wakiwemo watoto. Hii husaidia kila mtu kuhisi kuungwa mkono, kusikilizwa na kueleweka.
- zungumza na mtoto wako kuhusu jinsi watu wanaweza kukabiliana na shida. Mwambie hisia zake ni za kawaida katika mazingira haya. Unaweza kumhakikishia kwamba atajisikia vizuri baada ya muda.
Jinsi unavyoweza kuitikia tukio lililosababisha kiwewe
Mwitikio wako kwa hisia na tabia ya mtoto wako utaathiri kupona kwake au la. Ni muhimu:
- kuwa na ufahamu kuhusu mabadiliko yake ya tabia. Watoto huitikia matukio ya kufadhaisha au ya kutisha kwa njia tofauti. Mabadiliko katika tabia zao kama vile hasira au kukojoa kitandani ni kawaida.
- mpe mtoto wako umakini zaidi. Hii inaweza kuwa muhimu wakati wa kulala na wakati mwingine wa kujitenga.
- jipatie msaada. Watoto huwategemea wazazi au walezi wao ili kuelewa shida na jinsi ya kuitia. Wanahitaji watu wazima karibu nao kuelewa hofu zao na kuwafariji. Ikiwa una shida, unaweza kupata msaada pia. Usipofanya hivyo, inaweza kuongeza hofu na mafadhaiko ambayo mtoto wako anahisi.
- zungumza kuhusu hisia zako kwa njia ifaayo na mtoto wako. Hili linaweza kumsaidia kuzungumza kuhusu hali yao.
- kumbuka kuwa kila mtu ni tofauti na anaweza kuwa na hisia tofauti. Usitarajie mtoto wako kuhisi kama wewe.
- umpe mtoto wako hisia ya udhibiti wa maisha yake. Hata kufanya maamuzi madogo kunaweza kumfanya ajisikie ana udhibiti zaidi. Hii ni muhimu hasa baada ya machafuko ya mgogoro. Watoto ambao wanahisi kutokuwa na uwezo wanaweza kupata mkazo zaidi.
- jaribu kutomlinda mtoto wako kupita kiasi. Ni kawaida kwako kutaka kuweka familia yako karibu baada ya shida. Lakini ni muhimu kuwasaidia kuhisi kwamba ulimwengu wao ni mahali salama pa kuwa.
Taratibu za familia baada ya tukio la kiwewe
Ni muhimu:
- kuendelea na utaratibu wako wa kawaida kadri uwezavyo. Hii inatia moyo kwa watoto.
- mhakikishie mtoto wako ikiwa hawezi kudhibiti utaratibu wake wa kawaida. Hii inaweza kujumuisha kuhudhuria shule au kufanya kazi za nyumbani.
- epuka kuleta mabadiliko kama vile taratibu mpya, majukumu au matarajio ya tabia zake.
- dumisha jukumu lako kama mtu mzima nyumbani. Ikiwa unahangaika, ni muhimu usitegemee msaada wa mtoto wako.
Jinsi ya kumsaidia mtoto wako kupona:
Ni muhimu:
- kuruhusu mtoto wako muda wa kutosha wa kucheza. Hii inaweza kuwa mchezo, michezo anayopenda na shughuli na marafiki anaowajua.
- kuruhusu muda kwa ajili ya kujifurahisha. Vicheko, nyakati nzuri na furaha ya pamoja vinaweza kusaidia wanafamilia wote kujisikia vizuri.
- kumbuka kwamba hamu ya mtoto wako inaweza kubadilika. Ikiwa hataki kula wakati wa chakula, umpe vitafunio vya kawaida siku nzima badala yake.
- hakikisha mtoto wako anapumzika vya kutosha na kulala.
- msaidie kufanya mazoezi ya mwili. Hii itasaidia mtoto wako na matatizo na kuboresha usingizi wao.
- punguza sukari, vyakula vya rangi na chokoleti.
- msaidie mtoto wako kupumzika kimwili. Hii inaweza kuwa na kuoga maji ya joto, masaji, nyakati za hadithi na kubembelezana.
- badilisha shughuli ikiwa inamfanya mtoto wako afadhaike au kuwa na wasiwasi. Kwa mfano, kipindi cha televisheni ambacho humfanya mtoto wako awe na wasiwasi au hofu.
Ikiwa wakati wowote una wasiwasi kuhusu afya yako ya akili au afya ya akili ya mpendwa wako, pigia simu Lifeline kwa 13 11 14.
Mahali pa kupata msaada
- GP (daktari) wako
- Muuguzi wako wa afya ya mama na mtoto
- Kituo chako cha afya cha jamii kilicho karibu nawe
- Daktari wa Watoto au Daktari wa Saikolojia ya Mtoto na Vijana - daktari wako anaweza kukuelekeza
- Kituo cha Phoenix Australia cha Afya ya Akili ya Baada ya Kiwewe Simu. (03) 9035 5599
- Kituo cha Huzuni na Msiba Simu. 1800 642 066
Unaweza pia kupata ushauri kutoka kwa:
- Lifeline Simu. 13 11 14
- GriefLine Simu. 1300 845 745
- beyondblue Simu. 1300 22 4636
- Kids Helpline Simu. 1800 55 1800
- MUUGUZI-WA-ZAMU Simu. 1300 60 60 24 – kwa maelezo ya afya ya kitaalam na ushauri (saa 24, siku 7)
- Tovuti ya Wazazi ya Australia – raisingchildren.net.au